Haihitaji kuwa na eneo kubwa ili uanzishe bustani. Bustani ya mboga mboga nyumbani kwako sio tu itakuletea muonekano mzuri wa nyumba yako kwa nje lakini pia, itakusaidia kupata chochote kiendacho kinywani.
Ugumu wa maisha na kupanda na kushuka kwa bei ya vyakula hufanya watu wale mlo mmoja. Lakini unapopata hela ya mboga ukaitunza sababu mboga ziko shambani, basi hiyo akiba unaweza inunulia nyama. Hahah! Hudumia familia yako basi.
Anzisha shamba la matunda na mboga mboga. Anzisha shamba dogo la kile uwezacho. Waweza kuwa na la mchicha au matembele tu kwa kuanzia. Tunza hela kwa kununua mboga kila siku ambazo unaweza zipata kwako. ZAIDI, utakuwa unapata klilicho salama zaidi
No comments:
Post a Comment