MAHITAJI
- Viazi ulaya
- Nyama ya kusagwa
- Kitunguu swaumu
- Kitunguu maji
- Hoho
- Karoti
- Mafuta ya kupikia
- Mayai
- Pilipili (ukitaka)
MAANDALIZI
- Menya viazi
- Vioshe na maji safi
- Menya na twanga kitunguu swaumu
- Katakata viungo vipande vidogo vidogo
- Pasua majai weka kwenye chombo kisafi kisha koroga na chumvi kwa mbali
MAPISHI
- Chemcha viazi viive
- Twanga au ponda ponda vilainike
- Chemsha nyama na chumvi kwa mbali
- Ikiishaiva weka kitunguu swaumu, kitunguu maji, hoho, karoti na pilipili ukitaka
- Changanya viungo vyako kwa pamoja vichanganyike vizuri (hakikisha hakuna maji bali mvuke)
- Weka viazi ulivyoisha viponda
- Changanya vyote kwa pamoja
- Chukua kidogo kidogo mkononi
- Finyanga kwa urefu
zikiwa tayari kwa kukaangwa |
- Tosa kwenye mayai
- Kaanga kwenye mafuta ya moto
zimeiva, tayari kwa kuliwa |
No comments:
Post a Comment