Tuesday, March 22, 2016

"Watu wenye ulemavu wanahaki ya usawa na kuheshimiwa".


Kuna ulemavu wa aina mbali mbali. Machache yajulikanayo ni kushindwa kutembea kushindwa kutumia mikono, kutoona vizuri ama kutoona kabisa, ulimi kuwa mzito hivyo kushindwa kuongea, kutosikia (kiziwi), mifupa kujikunja na kusababisha matege pamoja na kukosa melanin itengenezayo rangi ya ngozi (albino).

Watu wenye ulemavu wanapaswa kujijali pia, wanapaswa kupata lishe iliyo bora kabisa ili kujikinga na maradhi. Hawapaswi kujihurumia na kujitenga, bali kuwa na jamii yao, hivyo kuwa na afya ya mwili na akili na kuwa na amani.

Dk Abdallah Possi, Naibu Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu (Ofisi ya Waziri Mkuu) ni kijana mwenye albinism lakini anatumia fursa ya kuwa Naibu Waziri kuelimisha jamii zaidi juu ya watu wenye ulemavu na kuwaasa waachane na mtazamo potofu wa kulionea kundi hilo. 

Naibu Waziri anasema kuwa, ''kila mtu ni sawa lakini usawa huo uzingatie mtu na mtu; yaani, kila mtu aheshimiwe na kusikilizwa kulingana na nafasi ama hali aliyonayo''. Kundi la watu wenye walemavu limeonekana kuachwa nyuma kwani ni wachache na watu wengi wameonekana kuwaacha walio wachache na wale wachache wanajiona sio wa kawaida. 

Amesema, ili kutibu historia ya muda mrefu ya watu wenye walemavu kuachwa nyuma, haipaswi kuwepo kwa mtazamo wa upendeleo bali wachangamke ili kujitoa katika kundi walilomo kama ilivyokuwa katika swala la wanawake.

No comments:

Post a Comment