Wednesday, March 23, 2016

Fahamu kuhusu MAYAI

Je, unafahamu kuwa yai hulainisha koo?


Kama ilivyo kwa baadhi ya vyakula, yai hupoteza virutubisho linapopikwa iwe kwa kukaangwa ama kwa kuchemshwa.Yai lina Vitamin D ambayo hupungua pindi lipikwapo. Hupungua kwa asilimia 90 likichemshwa sana hivyo kupoteza umuhimu wake kwa mwili wa binadamu. Sasa basi, ili kupata virutubisho vyote vya yai ni muhimu kulila likiwa bado bichi.

 Mayai mabichi ni mazuri kwa kula ili kupata lishe sahihi lakini kwa wale wenye aleji (allergy) mayai mabichi si sahihi kwao kwani inaongeza athari zaidi. Mayai pia huweza kuwa na vijidudu (bacteria) waitwao Salmonella enteritidis (SE) ambavyo vinatokana na ndege mwenyewe mfano kuku. Ni vizuri kuchunguza yai kabla ya kula ili kuepukana na athari zinazoweza kujitokeza. Epuka kula mayai mabichi yaliyotagwa na kuku mgonjwa kwani ndio mwenye uwezekano mkubwa wa kuwa na SE.

Pata yai moja hadi mawili kwa siku. Yai halina shombo sana kwa hiyo ni rahisi kulinywa haraka likiwa bichi. Hizi ni faida za kula mayai kwa mwili wa binadamu:-
  • Mayai hupunguza athari ya tatizo la moyo kwa kiwango kikubwa sana.
  • Ni chanzo kizuri cha kupunguza protini iliyozidi mwilini.
  • Husaidia kuupa mwili mafuta kiasi yanayohitajika mwilini.
  • Huunguza na kupunguza kiwango cha mafuta yasiyohitajika mwilini.
  • Huondoa sumu iliyojificha mwilini.
  • Husaidia katika kuzifanya kucha na nywele kuwa ngumu.
  • Husaidia katika kuifanya mishipa  na damu kufanya kazi kwa uzuri kabisa.
  • Mayai yanasaidia kutunza kumbukumbu.
  • Mayai yanavirutubisho aina ya foleti (folate) ambayo imetengenezwa vidonge, navyo vinashauriwa kwa wajawazito kuvinywa ili kupata chembe hai za damu.
  • Huleta kinga nzuri ya mwili ambayo hupunguza uwezekano wa kupata kansa kwa kiwango kikubwa. 
  • Ni chakula bora chenye virutubisho vingi na vyenye kulingana (balanced diet).
  • Hufanya mfumo wa ubongo kufanya kazi vizuri.
  • Huleta usawa katika homoni (hormones).
  • Hulainisha misuli.
  • Huupa mwili nguvu zaidi.
  • Kwa wale wanywaji, mayai mabichi ni kiungo kizuri kuondoa hangover.
  • Inapunguza, kama sio kuondoa ngozi iliyoungua
Haishauriwi kutunza mayai katika friji ila yawekwe katika sehemu iliyopoa yaani ambayo haina joto kali wala baridi lililozidi. Ni muhimu kukagua yai kabla ya kulitumia hasa likiwa bichi; lakini sio tu kukagua mayai lakini kutumia mayai ya kienyeji kwani ndiyo yenye lishe zaidi.

Usile yai:-
  • lililopata ufa
  • lililotoboka
  • lenye harufu kali ama kidogo
  • lisilo na harufu kabisa ya yai
  • lililojepesi yaani halizami kwenye maji mfano kwenye bakuli
Njia nzuri ya kupata yai salama ni kwa kufuga kuku mwenyewe na kama hutaweza kwa sababu mbalimbali basi nunua mayai kwa mtu anayefuga mwenyewe ili kuwa na uhakika wa usalama wa afya yako.

4 comments:

  1. Vizuri mkuu Kwa Elimu nzuri na Ushauri Kwa manufaa Kwa Kila mmoja.ASANTE

    ReplyDelete
  2. Nimependezwa sana na nakala hii pia nimejifunza mimi pia ni mfugaji wa kuku wa mayai

    ReplyDelete