Nyanya ni tunda linaloliwa kwa njia mbali mbali. Wengine hutengenezea kachumbari, wengine huungia mboga, wengine hupikia rosti lakini wengine hupendelea kuisaga na kunywa juisi (juice).
Tunda hili linafaida sana katika mwili wa binadamu. Lakini zaidi ni kama litatumika likiwa na virutubisho vyake vyote; yaani, likiwa bado bichi.
Nyanya mbichi ni chanzo cha Vitamin A, Vitamin K, Vitamin B1, B2, B3, B5 na B6, pamoja na madini kama magneziam (magnesium), chuma (iron) na fosforas (phosphorus).
Tafiti mbalimbali zimefanyika na kugundua kuwa, nyanya hasa katika mfumo wa maji ama kimiminika (liquor), inafaida. Moja kwa moja tuziangalie faida za juice ya nyanya kwa ngozi, nywele na afya ya mwili.
- Hupunguza matatizo ya moyo.
- Hupunguza athari ya moshi wa sigara hasa ule uvutwao na mtu wa pili.
- Husaidia kuwa na mzunguko mzuri wa chakula.
- Husaidia kupata choo.
- Hufanya nywele kuwa ngumu na zenye afya.
- Huimarisha ngozi na kuifanya nyororo.
- Hupunguza hatari ya kuganda kwa damu.
- Huongeza kiwango cha kuunguza mafuta mwilini.
- Hulikinga jicho dhidi ya magonjwa na kulifanya lione vizuri.
- Hupunguza athari ya kansa kama vile: kansa ya matiti, kibofu, mapafu na kongosho.
- Huepusha gonjwa la mshituko (stroke).
- Huupa mwili nguvu kwani huuacha na maji.
- Hulipa ini nguvu.
- Huufanya uso kuondokana na mikunjo na chunusi.
Kabla ya kutengeneza tunda hili kwa chochote, hata kama litapikwa, hakikisha unaliosha kwa maji safi na salama kisha ulifute kwa kitambaa safi; ndipo ulitumie. Kitu cha kuzingatia ni usafi.
Jaribu kutengeneza juice ya nyanya, jizoeshe kuinywa walau mara moja kwa wiki uone mabadiliko yenye mafanikio katika mwili wako.
No comments:
Post a Comment