Wewe ni wa muhimu!!! Jifunze umuhimu wako wewe kama binadamu kama utazingatia afya bora kwako na kwa mwenzako.
Kula chakula chenye lishe na kufanya mazoezi ni changamoto kwa wengi hasa ukizingatia mfumo wa maisha kwa wengi hivi sasa. Lakini, ni afya njema tu itakayokupa nguvu ya kufanya yaliyo mazito na wepesi wa kufanya yaliyo magumu.
Lishe inayoenda na mazoezi kiasi itakuepusha wewe na magonjwa kama kisukari, presha ya damu, unene wa kupindukia, kansa na mtindio wa ubongo. Badala yake hukupa vitu kama upeo mzuri wa kufikiri, nguvu, amani, wepesi, mzunguko mzuri wa damu na wa chakula, kwa kutaja machache.
Mstari mmoja wa kitabu cha dini unasema "Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa". Usijiachie ukasahau kutunza afya yako kwani wewe ni wa muhimu sana katika ulimwengu huu. Mungu hakukosea kukuumba hivyo ishi kwa kujali afya yako ili uwe na maisha yenye furaha. Magonjwa hututoa furaha, unene hutunyima uhuru kufanya baadhi ya vitu, kwa nini basi tusijitunze kwa kuzingatia lishe na mazoezi ili kupata afya na nguvu tele?!
Usiwe nyuma katika kujua afya yako, pima mara kwa mara na ufanye tafiti hasa kwa kusoma nyaraka mbali mbali za afya ili uwe kwenye njia sahihi.
No comments:
Post a Comment