Ninajijali, wewe je?
Tunajijali, wewe je?
Wewe ni wa muhimu hivyo jijali muda wote. Zingatia lishe bora na uchangamshe mwili wako kwa mazoezi kiasi. Furahi, afya ya akili huupa mwili afya pia. J. A. Y!!
Wednesday, March 23, 2016
Wewe ni wa muhimu
Wewe ni wa muhimu!!! Jifunze umuhimu wako wewe kama binadamu kama utazingatia afya bora kwako na kwa mwenzako.
Kula chakula chenye lishe na kufanya mazoezi ni changamoto kwa wengi hasa ukizingatia mfumo wa maisha kwa wengi hivi sasa. Lakini, ni afya njema tu itakayokupa nguvu ya kufanya yaliyo mazito na wepesi wa kufanya yaliyo magumu.
Lishe inayoenda na mazoezi kiasi itakuepusha wewe na magonjwa kama kisukari, presha ya damu, unene wa kupindukia, kansa na mtindio wa ubongo. Badala yake hukupa vitu kama upeo mzuri wa kufikiri, nguvu, amani, wepesi, mzunguko mzuri wa damu na wa chakula, kwa kutaja machache.
Mstari mmoja wa kitabu cha dini unasema "Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa". Usijiachie ukasahau kutunza afya yako kwani wewe ni wa muhimu sana katika ulimwengu huu. Mungu hakukosea kukuumba hivyo ishi kwa kujali afya yako ili uwe na maisha yenye furaha. Magonjwa hututoa furaha, unene hutunyima uhuru kufanya baadhi ya vitu, kwa nini basi tusijitunze kwa kuzingatia lishe na mazoezi ili kupata afya na nguvu tele?!
Usiwe nyuma katika kujua afya yako, pima mara kwa mara na ufanye tafiti hasa kwa kusoma nyaraka mbali mbali za afya ili uwe kwenye njia sahihi.

Fahamu kuhusu MAYAI
Je, unafahamu kuwa yai hulainisha koo?
Kama ilivyo kwa baadhi ya vyakula, yai hupoteza virutubisho linapopikwa iwe kwa kukaangwa ama kwa kuchemshwa.Yai lina Vitamin D ambayo hupungua pindi lipikwapo. Hupungua kwa asilimia 90 likichemshwa sana hivyo kupoteza umuhimu wake kwa mwili wa binadamu. Sasa basi, ili kupata virutubisho vyote vya yai ni muhimu kulila likiwa bado bichi.
Mayai mabichi ni mazuri kwa kula ili kupata lishe sahihi lakini kwa wale wenye aleji (allergy) mayai mabichi si sahihi kwao kwani inaongeza athari zaidi. Mayai pia huweza kuwa na vijidudu (bacteria) waitwao Salmonella enteritidis (SE) ambavyo vinatokana na ndege mwenyewe mfano kuku. Ni vizuri kuchunguza yai kabla ya kula ili kuepukana na athari zinazoweza kujitokeza. Epuka kula mayai mabichi yaliyotagwa na kuku mgonjwa kwani ndio mwenye uwezekano mkubwa wa kuwa na SE.
Pata yai moja hadi mawili kwa siku. Yai halina shombo sana kwa hiyo ni rahisi kulinywa haraka likiwa bichi. Hizi ni faida za kula mayai kwa mwili wa binadamu:-
Usile yai:-

- Mayai hupunguza athari ya tatizo la moyo kwa kiwango kikubwa sana.
- Ni chanzo kizuri cha kupunguza protini iliyozidi mwilini.
- Husaidia kuupa mwili mafuta kiasi yanayohitajika mwilini.
- Huunguza na kupunguza kiwango cha mafuta yasiyohitajika mwilini.
- Huondoa sumu iliyojificha mwilini.
- Husaidia katika kuzifanya kucha na nywele kuwa ngumu.
- Husaidia katika kuifanya mishipa na damu kufanya kazi kwa uzuri kabisa.
- Mayai yanasaidia kutunza kumbukumbu.
- Mayai yanavirutubisho aina ya foleti (folate) ambayo imetengenezwa vidonge, navyo vinashauriwa kwa wajawazito kuvinywa ili kupata chembe hai za damu.
- Huleta kinga nzuri ya mwili ambayo hupunguza uwezekano wa kupata kansa kwa kiwango kikubwa.
- Ni chakula bora chenye virutubisho vingi na vyenye kulingana (balanced diet).
- Hufanya mfumo wa ubongo kufanya kazi vizuri.
- Huleta usawa katika homoni (hormones).
- Hulainisha misuli.
- Huupa mwili nguvu zaidi.
- Kwa wale wanywaji, mayai mabichi ni kiungo kizuri kuondoa hangover.
- Inapunguza, kama sio kuondoa ngozi iliyoungua
Usile yai:-
- lililopata ufa
- lililotoboka
- lenye harufu kali ama kidogo
- lisilo na harufu kabisa ya yai
- lililojepesi yaani halizami kwenye maji mfano kwenye bakuli
Tuesday, March 22, 2016
"Watu wenye ulemavu wanahaki ya usawa na kuheshimiwa".
Kuna ulemavu wa aina mbali mbali. Machache yajulikanayo ni kushindwa kutembea kushindwa kutumia mikono, kutoona vizuri ama kutoona kabisa, ulimi kuwa mzito hivyo kushindwa kuongea, kutosikia (kiziwi), mifupa kujikunja na kusababisha matege pamoja na kukosa melanin itengenezayo rangi ya ngozi (albino).
Watu wenye ulemavu wanapaswa kujijali pia, wanapaswa kupata lishe iliyo bora kabisa ili kujikinga na maradhi. Hawapaswi kujihurumia na kujitenga, bali kuwa na jamii yao, hivyo kuwa na afya ya mwili na akili na kuwa na amani.
Dk Abdallah Possi, Naibu Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu (Ofisi ya Waziri Mkuu) ni kijana mwenye albinism lakini anatumia fursa ya kuwa Naibu Waziri kuelimisha jamii zaidi juu ya watu wenye ulemavu na kuwaasa waachane na mtazamo potofu wa kulionea kundi hilo.
Naibu Waziri anasema kuwa, ''kila mtu ni sawa lakini usawa huo uzingatie mtu na mtu; yaani, kila mtu aheshimiwe na kusikilizwa kulingana na nafasi ama hali aliyonayo''. Kundi la watu wenye walemavu limeonekana kuachwa nyuma kwani ni wachache na watu wengi wameonekana kuwaacha walio wachache na wale wachache wanajiona sio wa kawaida.
Amesema, ili kutibu historia ya muda mrefu ya watu wenye walemavu kuachwa nyuma, haipaswi kuwepo kwa mtazamo wa upendeleo bali wachangamke ili kujitoa katika kundi walilomo kama ilivyokuwa katika swala la wanawake.
Monday, March 21, 2016
Faida za juice ya nyanya.
Unafahamu umuhimu wa nyanya katika mwili wa binadamu?
Nyanya ni tunda linaloliwa kwa njia mbali mbali. Wengine hutengenezea kachumbari, wengine huungia mboga, wengine hupikia rosti lakini wengine hupendelea kuisaga na kunywa juisi (juice).
Tunda hili linafaida sana katika mwili wa binadamu. Lakini zaidi ni kama litatumika likiwa na virutubisho vyake vyote; yaani, likiwa bado bichi.
Nyanya mbichi ni chanzo cha Vitamin A, Vitamin K, Vitamin B1, B2, B3, B5 na B6, pamoja na madini kama magneziam (magnesium), chuma (iron) na fosforas (phosphorus).
Tafiti mbalimbali zimefanyika na kugundua kuwa, nyanya hasa katika mfumo wa maji ama kimiminika (liquor), inafaida. Moja kwa moja tuziangalie faida za juice ya nyanya kwa ngozi, nywele na afya ya mwili.
Kabla ya kutengeneza tunda hili kwa chochote, hata kama litapikwa, hakikisha unaliosha kwa maji safi na salama kisha ulifute kwa kitambaa safi; ndipo ulitumie. Kitu cha kuzingatia ni usafi.
Jaribu kutengeneza juice ya nyanya, jizoeshe kuinywa walau mara moja kwa wiki uone mabadiliko yenye mafanikio katika mwili wako.

- Hupunguza matatizo ya moyo.
- Hupunguza athari ya moshi wa sigara hasa ule uvutwao na mtu wa pili.
- Husaidia kuwa na mzunguko mzuri wa chakula.
- Husaidia kupata choo.
- Hufanya nywele kuwa ngumu na zenye afya.
- Huimarisha ngozi na kuifanya nyororo.
- Hupunguza hatari ya kuganda kwa damu.
- Huongeza kiwango cha kuunguza mafuta mwilini.
- Hulikinga jicho dhidi ya magonjwa na kulifanya lione vizuri.
- Hupunguza athari ya kansa kama vile: kansa ya matiti, kibofu, mapafu na kongosho.
- Huepusha gonjwa la mshituko (stroke).
- Huupa mwili nguvu kwani huuacha na maji.
- Hulipa ini nguvu.
- Huufanya uso kuondokana na mikunjo na chunusi.
Kabla ya kutengeneza tunda hili kwa chochote, hata kama litapikwa, hakikisha unaliosha kwa maji safi na salama kisha ulifute kwa kitambaa safi; ndipo ulitumie. Kitu cha kuzingatia ni usafi.
Jaribu kutengeneza juice ya nyanya, jizoeshe kuinywa walau mara moja kwa wiki uone mabadiliko yenye mafanikio katika mwili wako.
Sunday, March 20, 2016
Saturday, March 19, 2016
Friday, March 18, 2016
Ongezeko la magonjwa pamoja na unene uliopindukia vinasababishwa na ukosaji wa elimu ya sayansi ya vyakula. Unafahamu aina ya vyakula? Unafahamu ni kiasi gani unapaswa kula chakula na kwa muda upi?
Baadhi wanauelewa lakini wamesahau. Wengine hawafahamu kabisa lakini wengi tunapuuzia kwani hatufuatilii kabisa.
Pitia blog hii mara kwa mara utambue ni nini na vipi unapaswa kula ili kuwa na afya njema. Utatambua magonjwa yaliyopo na yanayoibuka kwa kukosa lishe bora.

Thursday, March 17, 2016
Subscribe to:
Posts (Atom)