Endelea kukimbia hata kama ni wa mwisho katika mashindano. Huwezi jua, yawezekama ukawa bingwa.
Ninawakummbusha ndugu zanguni kutokata tamaa maana muda unaokata tamaa unaweza kuwa ndio muda sahihi kabisa kwa wewe kupata mafanikio/ ukitakacho/ ulichoomba kwa muda mrefu/ kufikia ndoto zako na kadhalika.
Ukihisi kuacha usiache, kazana kwa kuwa umekaribia. Sote ni washindi kwa muda tofauti na kwa namna tofauti.
Wewe ni wa muhimu hivyo jijali muda wote. Zingatia lishe bora na uchangamshe mwili wako kwa mazoezi kiasi. Furahi, afya ya akili huupa mwili afya pia. J. A. Y!!
Friday, July 22, 2016
Thursday, July 21, 2016
Kila lililokamilika huanza kwa uamuzi wa kujaribu.
Msemo wa leo ni wa kutuhamasisha zaidi. Kila lililokamilika huanza kwa uamuzi wa kujaribu.
Chukua mfano huu mdogo. Umekaa kochini ukatamani maji ya kunywa lakini unaona uvivu kunyanyuka, hutapata maji. Kuna watu ndani unashindwa kuwaomba msaada wakuletee, hutapata maji. Umepata ila ni ya moto unahitaji ya baridi na huchukui uamuzi wowote, hutakata kiu yako.
Sasa, unataka kufanikisha mipango yako ambayo pengine hujaanza hata kujipanga, hutaikamilisha. Inatakiwa ifikie wakati ambapo utasimama hata kama umechoka au hujiwezi kufedha au kimwili. Anza safari huku ukiomuomba Mungu, naye atakuimarisha ukiwa njiani na utafika salama.
Fanya maamuzi haraka ya wapi uanze ama wapi upite na sio maamuzi ya kuendelea kusubiri. Bora ujaribu ushindwe kuliko usijaribu kumbe unajikosesha faida. Na ukijaribu ukashindwa usikate tamaa haraka, jaribu tena na tena mpaka utakapoona haiwezekani kabisa; ingawaje hakuna lisilowezekana kwa Mungu. Utachelewa lakini sio kushindwa.
Kazi kwako...
Wednesday, July 20, 2016
Onyesha heshima hata kwa watu wasiostahili; sio kwa muonekano wa tabia zao ila muonekano wa yako.
Inakuwaje mtu hastahili heshima yako? Ni kwa sababu haonyeshi upendo kwako kama binadamu, sababu anakuona uko chini sana, sababu anakudharau, anakuona hufai kwake na katika maisha yake, sababu huna uwezo kifedha ama kifikra, sababu huwezi kufika alipofika, sababu hujampa alichotaka, hauna muonekano mzuri na mengine mengi.
Zipo sababu nyingi lakini pamoja na yote tunapaswa kukumbuka kuwa sote ni binadamu na tunakosea. Inawezekana tukapishana leo lakini tukumbuke dunia huzunguka, binadamu pia. Tuheshimiane kwani hatujui ya kesho, inawezekana ukamheshimu mtu leo hata kama hastahili na kesho akawa msaada mkubwa tu kwako. Lakini tukijikweza leo, kesho tutaaibika.
Usimuhemu huyu ukamuacha yule ukidhani unakuwa mwema zaidi. Heshimu wote ili uonekane mwenye heshima.
AFRITRACUL
Tuesday, July 12, 2016
AFYA ni nini?
Afya ni hali ya kutokuwa na ugonjwa au kidonda. Afya ni hali ya kuwa na amani ya roho. Afya ni ubora wa akili, mwili na nafsi. Afya hutegemea vitu hivi vitatu kuwa ili kuwa hai na salama:
- Akili
- Mwili
- Nafsi
Akili ni utashi tuliopewa na Mwenyezi Mungu katika kung'amua mambo ulimwenguni. Akili hujumuisha uelewa, ufikiri, uamuzi na utendaji wa mambo. Hakuna awezaye kutafsiri akili yetu ila matendo yetu yanaweza kumfanya mtu aone flani yuko vipi; nayo bado itakuwa mtazamo wake sababu tunatofautiana kufikiri pia.
Binadamu hutumia akili kila siku na kila wakati ili kuelewa, kufikiri, kuamua na kuhakikisha tunatimiza jambo. Kwa maana hiyo, tunapaswa kuipumzisha "PUMZISHA AKILI". Akili ikichoka mwili nao huchoka na hutafanya chochote sababu haitakuwa na uwezo mzuri kutenda. Lala au oga au ogelea au sikiliza mziki au chochote ukipendacho ambacho hakitakufanya utumie nguvu ya akili.
Mwili ni muundo wote wa binaadam. Ni maumbile ya mtu. Mwili huhusisha yote yaliyotengeneza "mtu" mfano viungo kama miguu, mikono n.k, Maji kama mate, damu n.k, na vingine kama mishipa kucha na nywele.
Tunapaswa kujipenda kwa kula vizuri, kulala vizuri na pazuri, kuvaa vizuri na kujijali muda wote kwa kuuweka mwili salama mfano kwa kupiga mswaki baada ya kula, kuosha nywele mara kwa mara, kukata na kusafisha kucha, kuoga, na kuvaa nguo safi. Pia tujiepushe na hatari, ugomvi na makwazo kwa faida ya mioyo yetu.
Ukitembea sana juani pata kivuli unywe na maji. Penye baridi uvike mwili wako kwa sweta ama nguo nzito. Ukiumia au kuumwa pata matibabu sahihi kwa kwenda hospitalini. Jipende, Ujali mwili wako. Tukifanya hivyo miili yetu itakuwa salama.
Nafsi ni roho yenye kuleta imani ndani yetu. Sisi huamini vitu mbali mbali kwa msaada wa nafsi. Lakini yote heri kama tutaamini vitu vyenye kujenga na sio kubomoa. Nafsi pia hutofautiana ya mtu na mwingine ndio maana tukawa tofauti japo chimbuko letu kiuumbaji ni moja.
Nafsi nayo huhitaji utulivu ili kuupa mwili na akili nguvu za kuishi kwa afya. Pata muda wa kutulia ukiongea na WEWE kujua nini waweza fanya LAKINI, mshirikishe MUUMBA wako kwa yote kupata amani uitakayo moyoni na kwa wakuzungukao.
Hivyo basi, jipe likizo au omba likizo. Tembelea sehemu mbali mbali za starehe au vivutio kutuliza mwili, akili na roho pia. Ongea vizuri na watu, cheka, tabasamu hata kama umeumizwa. Inasaidia sana.
Afya ya vitu vyote vitatu ni muhimu katika kukuweka mwenye nguvu na furaha.
Monday, July 11, 2016
Friday, July 8, 2016
KUWA MTU MZURI LAKINI USIPOTEZE MUDA KUTHIBITISHA
Tumeumbwa tupendane lakini haimaanishi umpende kila mmoja sawa sawa. Tunapaswa kusaidiana na kuheshimiana lakini inaposhindikana unaacha. Usiumize kichwa kumfurahisha asiyetaka au asiyestahili. Kakupotezea muache, usimlete karibu kilazima.
Asipokuona mzuri machoni mwake muache sababu wapo wengine maelfu zaidi wanaokuona uko sawa. Hajaona thamani yako muache sababu wapo wengi zaidi wanaotambua uwepo wako na hasa umuhimu wako.
Timiza wajibu wako kwa kila mmoja katika jamii yako kulingana na nafasi yako kwao. Jali, heshimu, penda, sahihisha, funisha, ongoza, furahisha, onya, lakini kama haionekani kumsaidia unayemfanyia badilisha njia, mtazamo, suluhisho, matendo. Usilazimishe wala kung'ang'ania, utajiumiza.
Yamkini mia wakakusema vibaya, usiumie sababu yupo japo mmoja anayetambua uzuri wako kwa wema wako; na hilo ni kuu mno. Kuwa hivyo ulivyo na uache mengineyo yapite njia yake...
Subscribe to:
Posts (Atom)









